Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 04Article 540904

xxxxxxxxxxx of Friday, 4 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

RC Shigella ataka mapinduzi ya kilimo

MKUU wa Mkoa (RC) wa Morogoro, Martine Shigella, amesema ajenda kubwa ya mkoa ni kuleta mapinduzi ya maendeleo vijijini katika kilimo na ufugaji ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza kipato cha wananchi.

Shigella alisema katika kuleta maendeleo, mkoa utashirikiana na taasisi mbalimbali za umma ikiwa ni pamoja na kukitumia Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

"Mkoa wa Morogoro una fursa nyingi za maendeleo, nashukuru serikali zote tangu ya Awamu ya Kwanza hadi iliyopo sasa (Awamu ya Sita) zimefanya kazi nzuri kuwaleta wananchi maendeleo, " alisema Shigella.

Alisema utekelezaji huo hasa katika sekta ya kilimo ni pamoja na kusimamia kilimo kwa vitendo na kuendeleza mkoa huo kuwa ghala la taifa la chakula.

Kwa mujibu wa Shigella, mpango wa serikali wa usambazaji wa umeme vijijini pia umechangia kuharakaisha maendeleo ya wananchi yakiwemo ya ukuzaji wa sekta ya kilimo, mifugo na nyingine ikiwa ni pamoja na vijana kuendelea kubaki vijijini wakizalisha mali na kujipatia vipato.

Katika hatu nyingine alitaka Manispaa ya Morogoro ijipange vizuri kutumia fursa ya Treni ya Kisasa(SGR), inayotarajiwa kuanza safari hivi karibuni ili wakulima na wafanyabiashara wasafirishe bidha na mazao kwendakatika masoko yakiwamo yaliyopo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Uzalishaji), Dk Rozalia Rwegasira, alisema katika msimu wa mwaka 2019/2020 tani 2,016,332.20 zilizalishwa na mahitaji yalikuwa tani 629,112. 86.

Join our Newsletter