Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552274

Habari za Mikoani of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

RC Tabora azindua baraza la biashara la Mkoa

Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani

Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amezindua baraza la biashara manispaa ya Tabora na kuagiza lianze kutumika ndani ya Siku saba kuanzia sasa kama Jukwaa la kujadili na kutatua changamoto zinazoleta ukinzani baina ya Sekta binafsi na Serikali.

Baraza la Biashara ni mkakati wa Serikali kutambua umuhimu wa Sekta binafsi namna inavyoweza kuchangia pato la Taifa kwa kulipa kodi, Serikali imeona ni muhimu kuwa na barazala wafanyabiashara ikiwa ni njia moja wapo itakayosaidia kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na kisha kuweka mazingira wezeshi.

Akizindua baraza hilo katika manispaa ya Tabora Mkuu wa mkoa Dkt. Batilda Buriani ameagiza baraza hilo lianze mara moja kusikiliza kero za wafanyabiashara

Kwaupande wao baadhi ya wafanyabiashara wametoa wito kwa Serikali kuliimarisha Baraza hilo ili liweze kufikia malengo yaliyokusudiwa na si kuweka historia ya kulizindua na kulitekeleza kwakuwa wao wanaona ni jukwaa litakalowasaidia kukutana na mamlaka mbalimbali za Serikali na kupata msaada ama ufumbuzi wa masuala yanayokwamisha maendeleo yao.