Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 28Article 540343

xxxxxxxxxxx of Friday, 28 May 2021

Chanzo: millardayo.com

RC mpya Kilimanjaro aombwa kuanza na rushwa na ulevi

Viongozi mbalimbali wa dini mkoani Kilimanjaro wametoa malalamiko kwa Serikali ya Mkoa huo ya kukithiri kwa vitendo vya rushwa katika taasisi za afya na jeshi la polisi, Jambo ambalo limekuwa limekuwa likizorotesha juhudui za serikali za kutoa huduma bora kwa wananchi.

Pia viongozi hao wamemtaka Mkuu wa Mkoa huo, Stephen Kagaigai kuanza majukumu yake ya kwanza na suala la kudhibiti unywaji wa pombe za kienyeji aina ya gongo ambayo imekuwa ni changamoto kubwa katika baadhi za wilaya za mkoa wa huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wakati akitoa kero zao mbele ya mkuu huyo mpya wa mkoa,ambapo walisema kumekuwa na kero nyingi ambazo zimekuwa zikisababisha na watendaji wa zembe wasio jali wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya Askofu wa jimbo kuu katoliki la Moshi, Padre, Dk. Aidan Msafiri amesema vitendo vya rushswa Katika taasisi za umma vinapaswa kudhibitiwa kutokana na kwamba vimekuwa vikiathiri utendaji wa serikali Katika kuwa hudumia wananachi.

“Mkuu wa mkoa wakati umeingia hapa mkoani hapa tunaomba uanze na kushughulia masuala ya rushwa katika taasisi zetu za umma kwani baadhi ya watumishi wamekuwa wakisababisha Serikali kusemwa vibaya na wakati tunajua juhudi za Serikali katika utoaji wa huduma” Padre, Dk. Aidan Msafiri

“Pamoja na tatizo hilo pia tatizo la unywaji wa pombe uliokithiri katika mkoa huu ni kubwa hali ambayo imekuwa ni changamoto kwa vijana kutojishughulisha na shughuli za maendeleo tunaomba utusaidie katika hili,” Padre, Dk. Aidan Msafiri

“WALE WAARABU WANAOJENGA BWAWA LA UMEME WAKIMALIZA, NANI ATABAKI KU-MAINTAIN ULE MRADI” JENISTA

Join our Newsletter