Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 24Article 573868

Habari Kuu of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

RIPOTI: FAO yaagiza nchi zenye akiba ndogo ya chakula kujiandaa na majanga

RIPOTI: FAO yaagiza nchi zenye akiba ndogo ya chakula kujiandaa na majanga RIPOTI: FAO yaagiza nchi zenye akiba ndogo ya chakula kujiandaa na majanga

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetoa ripoti yake ya mwaka na kuonesha kuwa Janga la Covid-19, mabadiliko ya tabia nchI na migogoro kwa mara nyingine tena imekuwa na athari kubwa kwa usalama wa chakula, hasa katika bara la Afrika.

"Kuenea kwa njaa kumeongezeka katika Afrika Kaskazini," ripoti inabainisha "hasa ​​kutokana na kuongezeka kwa kiwango cha migogoro na ukosefu wa utulivu". Mabadiliko ya tabia nchi pia yanahusika.

Katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, zaidi ya watu milioni 80 wanaweza kukosa tena kupata Chakula chenye virutubisho vya kutosha vya lishe katika tukio la janga lingine, inaonya FAO. Katika nchi hizi, kusambaza utegemezi kati ya uzalishaji wa ndani na uagizaji wa bidhaa kutoka nje ni muhimu ili kupunguza hatari, inabainisha.

Kipengele kingine kilichoangaziwa: uwezo wa nchi kusafirisha bidhaa za chakula. FAO hata hivyo imeweka kiashirio kipya cha kutathmini uthabiti wa mitandao ya usafiri. Katika tukio la kufungwa kwa njia muhimu, kwa mfano: sehemu ya watu walioathirika inaweza kutofautiana kutoka 25% nchini Nigeria hadi 78% nchini Afrika Kusini.

Hatimaye, kilimo katika bara hili kinategemea zaidi biashara ndogo na za kati, ambazo mara nyingi sio rasmi lakini zimeunganishwa vizuri. biashara hizi zinabadilika kwa urahisi zaidi kwa mahitaji ya ndani. Lakini mara kwa mara zinanakumbana na vikwazo vya kitaasisi na ukosefu wa rasilimali. Pia ni dhaifu zaidi mbele kwa majanga. Mara nyingi, zinakabiliwa na tatizo la kupatikana kwa mkopo au ulinzi wa kijamii, limeongeza shirika hili la Umoja wa Mataifa.

"Leo kuna watu bilioni tatu hivi ambao hawawezi kumudu lishe bora. Kwa takwimu hizi lazima waongezewe watu bilioni moja ambao wanaweza wakajiunga na safu zao ikiwa janga litawanyima theluthi moja ya mapato yao, "ripoti hiyo imesema.