Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552520

Diasporian News of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: millardayo.com

Rais Mwinyi afanya Uteuzi Zanzibar Agosti 19, 2021

Rais Mwinyi afanya Uteuzi Zanzibar Agosti 19, 2021 Rais Mwinyi afanya Uteuzi Zanzibar Agosti 19, 2021

Rais wa Znz na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) kuanzia tarehe 18 August 2021 na kumteua Ramadhan Mwalim Khamis kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo ambapo uteuzi huo umeanza Aug. 18 2021.

Rais Dr. Mwinyi pia amemteua Balozi Amina Salum Ali kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Takwimu Zanzibar kuanzia tarehe 16 August 2021, pia Rais wamefanya uteuzi wa Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu kama ifuatavyo…

Bibi Salma Haji Saadat ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu huku Bwana Ussy Khamis Debe akiteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Watu wenye ulemavu, uteuzi huu umeanza tarehe 18 August 2021.