Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 26Article 553855

Diasporian News of Thursday, 26 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Rais Mwinyi ateua wakurugenzi, mtathmini mkuu

Rais Mwinyi ateua wakurugenzi, mtathmini mkuu Rais Mwinyi ateua wakurugenzi, mtathmini mkuu

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, amefanya uteuzi wa wakurugenzi na mtathmini Mkuu wa Serikali katika Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Alhamisi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Mhandisi Zena Said, uteuzi huo umeanza unaanza 26, 2021.

Katika uteuzi huo, Rais Mwinyi amemteua Muchi Juma Ameir kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Miji na vijiji.

Rais Mwinyi amemteua pia Juma Ameir kuwa Mkurugenzi wa Idara ya upimaji na Ramani huku Khamisu Hamid Mohamed ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa idara ya Uendeshaji na Utumishi.

“Ndugu Tahir Mussa Omar , ameteuliwa kuwa Mthamini Mkuu wa Serikali. Uteuzi huo unaanzia leo,” imesema taarifa ya Katibu Kiongozi huyo.