Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 17Article 552019

Habari Kuu of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rais Samia Ahimiza Ushirikishwaji wa Wanawake SADC

Rais Samia akiwa kwenye mkutano wa SADC Rais Samia akiwa kwenye mkutano wa SADC

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amehutubia mkutano wa 41 wa wakuu wa nchi na serikali wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC.

Rais samia amesema amesema kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza katika nchi za SADC kuongozwa na Rais Mwanamke, hivyo kujitambulisha kwake katika mkutano huo kutaongeza msukumo kwa wanawake wengi zaidi kujiamini na kuhamasika kushiriki katika vyombo vya maamuzi.

Aidha amewasihi Viongozi wote wa jumuiya hiyo kushirikiana katika kuendeleza jitihada za kuwainua na kuwawezesha wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi.

Akiwa kama kiongozi mpya katika jumuiya hiyo ameahidi kutoa ushirikiano ili kusukuma ajenda za utegemeano, kwa kushughulikia changamoto na kutekeleza mipango na mikakati mabali mbali ya maendeleo.