Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 25Article 553585

Habari Kuu of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rais Samia: "Askari jengeni ukaribu na raia, wasipowaamini hawatoi taarifa"

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia, ameagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha wanatekeleza mpango wa jeshi hilo kuwa na makazi ndani ya raia, ili kuweza kubaini na kudhibiti vitendo vya ugaidi na uhalifu.

Amewataka kufanya hivyo ili kujenga ukaribu na raia utakao wasaidia kudhibiti vitendo hivyo lakini pia kujenga imani kwa raia ili waweze kushirirkiana nao kwa wepesi.

"Magaidi wana mbinu za kukaa ndani ya raia, Jeshi la Polisi tukajenge urafiki na raia, tukakae huko ili wananchi watuambie nani ni nani, kuliko kutegemea tu taarifa kutoka kwa viongozi wa mtaa".

"Jamii isipokuwa na imani na Polisi hawatatoa taarifa, ni lazima tuwe na ukaribu na tujenge imani, hilo la jamii mliangalie"

Amesisistiza Jeshi hilo, kujengwa katika maadili ili watakapo ingia ndani ya jamii wajue mipaka ya kazi zao ili wasiingize urafiki na kazi kwa maendeleo ya taifa, ikiwa ni pamojana kuzingatia matumizi mazuri ya Polisi jamii katika utimizaji wa majukumu ya Jeshi hilo.