Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 25Article 553609

Habari Kuu of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rais Samia: "Inawezekana kupungua kwa kesi za jinai ni watu kukosa imani na jeshi la polisi"

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia, amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuangalia kwa kina sababu za kupungua kwa makosa ya jinai kuliko kufurahia, huenda watu wamekata tamaa kwenda vituo vya polisi kuripoti matukio mbalimbali.

Amesema jeshi hilo linatakiwa kusambaa zaidi kwenye jamii, kutoa huduma na kuzuia watu kutochukua sheria mkononi.

Akizungumza leo Jumatano Agosti 25, 2021 wakati akifungua kikao kazi cha maofisa wa jeshi hilo.

Samia amesema, "inawezekana kesi haziji vituoni kwa sababu watu wamekata tamaa kwa kuwa wakija hawapati haki zao."

“Wengine wanashindwa kwenda vituoni kwa sababu viko mbali hivyo watu kuamua kumalizana nyumbani na polisi mkafurahi kuwa mmepunguza makosa."

Pia amelipongeza jeshi hilo kwa kurudisha utulivu na usalama katika jiji la Dar es Salaam baada ya kukabiliana na hali ya sintofahamu iliyoanza kujitokeza.

“Wakati naingia kuna watu walitaka kujaribu, kazi imefanyika na sasa Dar es Salaam imetulia nasikia kesi chache tu huko mikoani. Sasa niwaombe wa mikoani nendeni mkafanye kazi nchi hii iepukane na vitendo vya unyang’anyi na ujambazi na ibaki salama,” amesema kiongozi mkuu huyo wa nchi.