Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 17Article 552037

Habari Kuu of Tuesday, 17 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Rais Samia: Mahitaji ya Chanjo ni makubwa nchi za SADC

Rais Samia Suluhu Hassan Rais Samia Suluhu Hassan

RAIS Samia Suluhu, amesema mahitaji ya chanjo ili kukabiliana na mlipuko wa janga la Corona ni makubwa na katika ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Kutokana na hali hiyo, Rais Samia amewataka wakuu wa nchi wa jumiya hiyo kuwa na sauti moja kwa kushawishi makampuni yanayotengeneza chanjo kutoa kibali na ujuzi ili nchi nyingine ziweze kuzalisha chanjo hizo.

Rais Samia ameyasema hayo leo katika mkutano wa 41 wa Jumuhiya hiyo unaoendelea nchini Malawi.

Aidha Rais Samia, alitoa wito kwa wakuu hao kuungana pia na kuwa na sauti moja ili kushawishi mataifa yaliyoendelea kusamehe madeni ambayo ni makubwa kuliko kipato cha nchi, au kuongeza muda wa ulipaji wa mikopo kutokana na uchumi wa mataifa mengi ya Afrika kuathiriwa sana na janga la ugonjwa wa huo wa Corona.

Ameongeza kuwa kutokana na janga hilo kuendelea kuisumbua dunia, njia pekee ya kupunguza athari za janga hilo ni kutoa chanjo kwa wananchi wa SADC.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa SADC aliyemaliza muda wake, Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi amesema kuwa hakuna nchi itakayosema iko salama hadi pale mataifa yote yatakapokuwa salama, hivyo ushirikiano ni muhimu katika kukabiliana na athari za Corona.