Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559933

Habari Kuu of Monday, 27 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Rais Samia: Sijawateua Kuwa Miungu Watu - Video

Rais Samia: Sijawateua Kuwa Miungu Watu - Video play videoRais Samia: Sijawateua Kuwa Miungu Watu - Video

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi wa mamlaka za serikali za mitaa kutenda haki na kuacha kuonea wananchi, kwani kwa kufanya hivyo wanajichumia laana.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 27, 2021, Jijini Dodoma, aliposhiriki Mkutano Mkuu Maalum wa viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), na kuongeza kuwa baadhi ya viongozi hao wamekuwa sehemu ya matatizo na kero za wananchi kwani hawatimizi majukumu yao.

“Nilisema sitaki kuona mabango yenye masikitiko, mabango ya shukrani acha wananchi waandike, mabango yenye masikitiko maana yake viongozi baadhi yenu hamtimizi majukumu yenu, mmekuwa ni sehemu ya kero kwa wananchi, nendeni mkajitathimini mjirekebishe.

“Kuna baadhi yenu hamuheshimiani, hamusikilizani nendeni mkaheshimiane, DC anasema hili DAS wake anasema hili, DED anasema hili mwingine anasema hili, mnavutana kwasababu fedha zinapoingia kila Mtu anataka amege fungu atie mfukoni mmoja akikataa mivutano inaanza.

“Tumepeleka kule watu wakatumikie wananchi, hujaenda kule kuwa Mungu wa wananchi, kama mimi ninawatumikia wananchi nategemea nawe niliyekuteua utakwenda kunisaidia kutumikia wananchi na sio kwenda kuwatesa wananchi.

“Simama kwenye haki, ulimwenguni unapita tu, na wote hapa tutakwenda kuulizwa, ulipata madaraka ya kuwahudumia wananchi ulifanya nini?, usiposimama kwenye haki laana inakuanza hapa duniani kwa Mungu unaenda kumalizwa…

“Wengine mkifika huko mnakuwa miungu watu, Baraza la Madiwani linakaa linaamua hivi wewe unasema unakwenda kivyako, mipango yote inayotekelezwa ifuate mipango na maagizo ya Kitaifa, sio kila mtu kupanga yake, kama anafanya hivyo achukue njia nyake.

“Watu ni wengi mno wanaosubiri hizo nafasi natoa, naweka wengine ambao wataenda kujituma na kutumikia wananchi… najua kuna wanaonitazama nilivyo na wakasema huyu mama hamna kitu… sasa tumesomana kazi iendelee,” amesema Rais SamiaSuluhu.