Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 14Article 563320

Habari Kuu of Thursday, 14 October 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Rais Samia: Takukuru Ng’ata, awashukia RC, RAS, DC ubadhilifu Bil.65.5/-

Rais Samia: Takukuru Ng’ata, awashukia RC, RAS, DC ubadhilifu Bil.65.5/- Rais Samia: Takukuru Ng’ata, awashukia RC, RAS, DC ubadhilifu Bil.65.5/-

RAIS Samia Suluhu amemuagiza Waziri Mkuu Kasssim Majaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), kuchukua hatua kwa wote watakaobainika kusababisha hasara ya sh bilioni 65.5 ya miradi 49 iliyobainika kuwa chini ya kiwango.

Rais Samia ameyasema hayo katika Kilele cha Mbio za Mwenge ambazo zimekwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 22 ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere wilayani Chato.

“Ni lazima tuunge nguvu katika kuikataa rushwa, miradi 49 yenye dosari mbali mbali ina viashiria vya ubadhirifu na iliyotekelezwa chini ya kiwango iliyosababisha hasara sh bilioni 65.5

“Ukiangalia kwa undani utakuta rushwa ni moja ya sababu kuu ya miradi hiyo kutotekelezwa ipasavyo.” amesema Rais Samia na kuongeza

“Ni imani yangu ofisi ya Waziri Mkuu, Takukuru, na Wizara zinazosimamia sekta husika, zitaifanyia kazi taarifa hiyo, na kuchukua hatua bila kumuonea mtu huruma wala muhali, na ikibainika waliofanya uzembe kutokana na vitendo vya rushwa hatua stahiki zichukuliwe.” amesema

Aidha alihoji “Najiulizwa kwa nini? viongozi wa maeneo hayo, Wakuu wa Mkoa, Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya, Takukuru, RSOs, DSOs wanasubiri mpaka Mwenge upite kujua dosari kwa nini kuna hilo tatizo, miradi yote inajengwa wakuu wote hao wapo, na hatua zozote hazichukuliwi kwa nini?

“Hiyo inatokana na kuwa hakuna ufuatiliaji, wakati miradi hii inatekelezwa. Naomba nitoe taadhari, kwenye miradi tuliyozindua juzi (Fedha za Benki ya Dunia) jambo hili lisijitokeze. kama nilivyosema nitasimama imara kutekeleza miradi ile na miradi mingine.

“Sitaki kuona dosari nyingi za miradi mwakani, na mikoa itakayokuwa na dosari Wakuu wa Mkoa, Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya, mjiandae, sitakuwa na mzaha katika hili.” amesisitiza

Kauli ya Rais Saamia imekuja baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, awali akitoa taarifa ya shughuli za Mwenge wa Uhuru amesema miradi jumla ya miradi 49 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 65.5 imekataliwa na kiongozi wa mbio ya Mwenge wa Uhuru 2021 Josephine Mwambashi baada ya kutiliwa shaka.

Mhagama alisema miradi hiyo iko katika wilaya 38 kati ya wilaya 150 zilizotembelewa na mbio za Mwenge mwaka huu.

"Miradi yote iliyotiliwa mashaka ya kuwepo vitendo vya ubadhirifu haikuzinduliwa wala kuwekewa mawe ya msingi kwa sababu viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru hawakutaka kujihusisha nayo na waliagiza Takukuru kufanya uchunguzi," amesema Waziri Mhagama

Ameongeza; "Taarifa ya uchunguzi wa miradi hii itawasilishwa kwako mheshimiwa Rais leo leo kwa uamuzi na maelekezo ambayo sisi tuko tayari kuyatekeleza,"

Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizozinduliwa Mei 17 na kuhitimishwa leo wilayani Chato umekagua na kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 1, 067 yenye thamani ya zaidi ya Sh1.2 trilioni. Miradi hiyo ni kutoka sekta za maji, nishati, afya, kilimo, uvuvi, mifugo na miundombinu.