Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585484

Habari Kuu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rais Samia: Tunzeni siri za Serikali

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi kufanya kazi kwa weledi na kutunza siri za Serikali kwa maslahi ya Taifa.

Akizungumza na mawaziri na manaibu katika Ukumbi wa Hazina leo Januari 13, 2022 jijini Dodoma, Rais amesema mara kadhaa imeonekana baadhi ya nyaraka za Serikali zikijadiliwa mitandaoni kitu ambacho ni kinyume na utaratibu.

"Imekuwa kama maradhi, nyaraka za Serikali tunazikuta mitandaoni, watu wanabishana huko mtu anaende kuchomoa ‘document’ inapigwa picha inawekwa kwenye mtandao, kama mnabisha ushahidi ni huo, hii haipendezi na hakuna serikali inaendeshwa hivyo,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amesema hali hiyo hairidhishi na kuwataka viongozi hao kuwa mfano na kuongeza kuwa siri zibaki ndani ya Serikali.

“Serikali inatoka kwenye ofisi zetu inaingia kwenye mitandao, kudhibiti siri za serikali, ziwe za siri 'classified' hata zile ambazo haziko 'classified', tunatakiwa mambo ya serikali yaishie ndani ya serikali," amesema Rais Samia.