Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 07Article 583945

Habari Kuu of Friday, 7 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rais Samia: Vijana Mkachanje

Rais Samia: Vijana Mkachanje Rais Samia: Vijana Mkachanje

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameshiriki Maadhimisho ya Kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibari, Wilaya ya Mkoani, Kusini Pemba leo tarehe 07 Januari, 2022.

"Uhai, usalama, maendeleo na ustawi wa Taifa lolote unategemea sana vijana, lakini hao ni vijana ambao wamelelewa vizuri, wamefunzwa itikadi na historia ya nchi yao, wakivikosa hivyo vyote fikiria itakuwa ni nchi ya namna gani"

"Niwaombe vijana mkachanje, chanjo zipo na ni bure, sikukuhakikishii kwamba ukichanja hutapata kabisa, hata kama utapata hautakuletea athari kubwa kidudu kikiingia, siku mbili tatu kinaondoka," – Rais Samia Suluhu leo kwenye kilele cha maadhimisho ya Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.