Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541726

xxxxxxxxxxx of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Rais Samia: Wanawake changamkieni fursa za kiuchumi kidijitali 

RAIS Samia Suluhu amesema kuna umuhimu wa kuziba pengo la kidijitali nchini kati ya wanawake na wanaume, kwa lengo la kuongeza fursa za ajira na kuliletea taifa maendeleo.

Amesema hayo leo wakati wa mkutano wake na wanawake, jijini Dodoma na kueleza kuwa idadi ya vijana wanaojiajiri kutumia mifumo ya kidijitali ni wengi ikilinganishwa na idadi ya vijana wa kike.

Rais Samia amesema tafiti zinaonesha kuwa kuna pengo kubwa kwenye matumizi ya mifumo hiyo kwa wanawake na wanaume, ambapo wanaume ni wepesi zaidi kutumia mifumo ya kidijitali kuliko wanawake.

Aidha amesema dunia ya leo inaendeshwa kwa mifumo ya kidijitali, na hivyo lazima vijana wasimame vizuri katika eneo hilo, na kuwa serikali inaenda kulifanyia kazi hilo.

Join our Newsletter