Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 22Article 552979

Habari Kuu of Sunday, 22 August 2021

Chanzo: millardayo.com

Rais Samia aagiza wanamichezo kupata chanjo ya COVID-19

Rais Samia Suluhu Hassan Rais Samia Suluhu Hassan

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Kombe la Ushindi la Michuano ya Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa Vijana wenye Umri chini ya Miaka 23 (CECAFA Challenge Cup 2021) viwanja vya Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

“Suala la chanjo ya Covid-19 ni muhimu, na wanamichezo kama hamjachanjwa naomba mkafanye, kwa kuwa mnasafiri sana, mimi Mama yenu, mkuu wenu, sitapeleka jamii yangu kwenye hatari, huwezi kushindana na mwanadamu mwenye kinywa, lakini ukweli ni kwamba chanjo hizi zinasaidia – Rais Samia

“Nimefurahia kupokea Kombe hili la CECAFA (U23) tunaamini kwamba kila safari huanza na hatua moja naamini ni safari ya kwenda kuchukua makombe mengine makubwa mbele ya safari ikiwa tu vijana hawa tutawatunza lakini ikiwa tutawaacha waende nyumbani Tukiwahitaji waje, hatutofika”-Rais Samia