Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 30Article 560545

Habari Kuu of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rais Samia aeleza umuhimu wa mashirika yasiyo ya kiserikali

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia amesema kuwa mashirika yasiyo ya kiserikali yana mchango mkubwa katika maendeleo pamoja na ustawi wa taifa kwa ujumla.

Ameyasema haya wakati akishiriki Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma leo Septemba 30, 2021.

Rais samia amesema kuwa mashirika haya yanafaida nyingi kwa jamii ikiwa ni pamoja na kuchochea maendeleo ya uchumi pamoja na kutoa nafasi za ajira kwa watu wengi jambo ambalo linaipunguzia mzigo taifa.

"Ni ukweli usiopingika kuwa mashirika yasiyo ya serikali yana mchango mkubwa kwenye maendeleo na ustawi wa taifa letu kwa mujibu wa takwimu nilizonazo hapa, zinaonesha kuwa mashirika yaliyosajiliwa ni 11603, yanayofanyakazi ni 4663 na jumla ya ajira zilizotokana na mashirika haya ni 17836" Rais Samia.

Amesisitiza kuwa mashirika haya yanachochea ukuaji wa uchumi wa taifa, kwani yanafanya kazi katika nyanja zote za uchumi na kijamii.

Amefafanua kuhusu mapato na matumizi ya mashirika haya kupitia uchambuzi uliofanyika mwaka 2020, na kubaini kuwa mapato yaliyotokana na mashirika yote yanayofanya kazi kuwa ni shilingi trilioni 1.2 huku matumizi yakiwa ni trilioni 1.

Aidha ameongeza kusema kuwa serikali mwaka 2001 ilitunga sera na sheria ambazo zinatumika kuongoza mashirika hayo, na kuwa sheria hizo zimeshafanyiwa marekebisho mara mbili kwa mwaka2005 na mwaka 2019.