Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 12Article 551206

Habari Kuu of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rais Samia afanya mazungumzo na Balozi wa Oman

Rais Samia akiwa na Balozi Ali Bin Abdallah Bin Salim Al Mahrouqi wa Oman Rais Samia akiwa na Balozi Ali Bin Abdallah Bin Salim Al Mahrouqi wa Oman

Mapema hii leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Oman hapa nchini, Ali Bin Abdallah Bin Salim Al Mahrouqi, aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Al Mahrouqi amempongeza Mhe. Rais Samia kwa utawala wake na kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa alioupata wakati alipokuwa akitekeleza majukumu yake nchini.

aliongeza kusema kuwa, Tanzania na Oman zina uhusiano mzuri na wa muda mrefu ambao umekuwa na matokeo chanya kwa mataifa yote mawili, hivyo ameomba uendelezwe kwa ajili ya maslahi ya pande zote mbili.

Kwa upande wake, Rais Samia, amemhakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendeleza na kudumisha ushirikiano wake na Oman kwa kudumisha amani na mshikamano kwa masalahi ya nchi zote mbili.

Mwisho kabisa, Rais Samia amemshukuru na kumpongeza Mhe. Balozi Al Mahrouqi kwa kazi nzuri ya uwakilishi wake hapa nchini katika kipindi cha miaka 4 kwa kudumisha uhusiano kati ya Oman na Tanzania.