Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541564

xxxxxxxxxxx of Monday, 7 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Rais Samia afuta mashamba 11 yenye ukubwa wa ekari 24,119 Kilosa, Morogoro

RAIS Samia Suluhu ameshusha neema kwa wananchi wa Kilosa kwa uamuzi wa kufuta jumla ya mashamba 11 yenye ukubwa wa ekari 24,119 katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro na kugawiwa kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo, ufugaji na uwekezaji.

Aidha, Rais Samia ameridhia ufufuaji wa mashamba 49 yenye ukubwa wa ekari 45,788.5 yaliyotaifishwa miaka ya nyuma huku na wananchi wakiwa hawana uhakika nayo ambapo Mhe. Rais ameelekeza sehemu kubwa ya mashamba hayo kutumiwa na wananchi kwa shughuli za kilimo.

Uamuzi huo wa Rais Samia umetangazwa leo Juni 07, 2021 wilayani Kilosa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza kwa nyakati tofati na viongozi, watendaji na wananchi wa kijiji cha Kimamba wilayani Kilosa wakati wa ziara yake mkoani Morogoro.

Hata hivyo, Waziri Lukuvi alisema pamoja na kufutwa mashamba hayo haimaanishi kama yako huru kwa kila mtu kujichukulia bila utaratibu na timu maalum imeundwa kwa ajili ya kupanga matumizi ya ardhi katika mashamba hayo na kutahadharisha asitokee mtu yeyote kuzuia timu hiyo kufanya kazi yake.

"Lazima tupange matumizi ya mashamba yaliyofutwa na utaratibu utaelekezwa na viongozi wa mkoa na wilaya na isitokee mtu kuja kujigawia mashamba na kila kipande cha ardhi kitapangwa na lazima ijukikane nani anamiliki" alisema Lukuvi.

Join our Newsletter