Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 09Article 541723

Habari Kuu of Wednesday, 9 June 2021

Chanzo: millardayo.com

Rais Samia akemea maiti kuzuiwa kisa madeni (+video)

Rais Samia akemea maiti kuzuiwa kisa madeni (+video) play videoRais Samia akemea maiti kuzuiwa kisa madeni (+video)

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuelekeza Waziri wa Afya,  Dk Dorothy Gwajima kuweka mpango mzuri wa ndugu kulipa deni la hospitali ili ikitokea  mgonjwa wao amefariki dunia wakati akitibiwa, maiti isizuiwe.

“Haileti maana mtu amefiwa anawaza msiba, kusafirisha na kuzika halafu bado unazuia maiti, hili haliwezekani.Nakuelekeza Waziri hebu nendeni mkaweke mpango mzuri wa kulipa deni na sio kuzuia maiti.” Samia

“Wananchi muelewe sio kwamba deni lisilipwe bali uwekwe mpango mzuri na mmoja wapo ni kulipa wakati matibabu yakiendelea na muhimu zaidi ni kuwa na bima ya afya,” Samia.