Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 25Article 573994

Habari Kuu of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rais Samia akiri kuzorota sekta binafsi, atoa maagizo kwa benki zote nchini

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Serikali imekiri kushuka kwa ukuaji wa sekta binafsi nchini kaika kipindi cha mwaka 2020/2021 hali iliyochangiwa na ongezeko kubwa la riba kwenye mikopo na inayotolewa na benki za ndani.

Rais Samia amethibitisha hili wakati akizindua Mkutano wa 20 wa taasisi za za fedha leo Novemba 25, 2021 jijini Dar es Salaam nakusema kuwa mikopo inayotolewa na benki nyingi haielengi kukuza sekta hizo.

Katika kufafanua hilo, Rais Samia amesema kuwa Benki Kuu imejitahidi kuonesha mfano kwa kuandaa mkakati wa kupunguza riba zake kwenye mikopo inayotolewa kwa sekta hiyo.

"Benki Kuu wameshaonesha njia na benki zingine waige mfano huu, shusheni kiwango cha riba ili sekta binafsi ziweze kukopa, nimeambiwa benki nyingine tayari wameshapunguza, na nyie mliobao jiongozeni mpunguze ili nazo ziweke kukopa na kukua" Amesema Rais Samia.