Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 30Article 554332

Habari Kuu of Monday, 30 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Rais Samia ameanza kurekodi vivutio vya utalii

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia Suluhu Hassan ameanza rasmi kurekodi kipindi kitakachotangaza Utalii, Biashara na Uwekezaji Nchini, Rais atatangaza kupitia Kipindi cha Royal Tour.

"Nimefuatana na wazungu wengi mtaona makamera makubwa hapa, wamekuja kuanza shughuli ya kuchukua vivutio mbalimbali nchini kwetu, mie ndio 'tour guide'" amesema Samia.

Rais Samia na wageni wa Royal Tour wameanza kazi ya kurekodi maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii na uwekezaji Agosti 28/2021 katika maeneo ya visiwa vya Zanzibar hasa Pemba na Unguja.