Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 10Article 569809

Habari Kuu of Wednesday, 10 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rais Samia ana nia njema na Machinga- Dkt. Mwigulu

Rais Samia ana nia njema na Machinga- Dkt. Mwigulu Rais Samia ana nia njema na Machinga- Dkt. Mwigulu

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba amesema kuwa Rais Samia ana nia njema na wafanyabiashara wadogowadogo 'Machinga' katika suala zima la kuwawekea mazingira bora ya kufanyia biashara.

Dkt Mwigulu ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja zilizochangiwa na baadhi ya Wabunge, amesema kuwa Rais Samia anataka kuwabadilisha wafanyabiashara hao kutoka kwenye kutumikishwa na wafanyabiashara wakubwa hadi kumiliki biashara zao wenyewe.

"Hiki wanachofanya sasa hivi wanatembea na bidhaa za watu kwasababu hatuwezi kuwafikia hata tukitenga hizo asilimia ngapi?hatuwezi kuwafikia,tunaamini wakishakuwa katika maeneo ambayo yatafikiwa wataweza kupata fedha kwenye saccos zao,wataweza kutembea na bidhaa zao, wataweza kuuza bidhaa zao" - amesema Waziri huyo.

Aidha amewataka Machinga wote kutulia kwani Serikali imejipanga kuwasaidia ili kufanikisha mipango yao, akifafanua hilo amesema kuwa Wizara ya Fedha inashirikiana na Wizara ya Ardhi ili kuwapanga wafanyabiashra hao kenywe maeneo yenye mvuto wa kibiashara.