Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 25Article 553693

Habari Kuu of Wednesday, 25 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rais Samia apokea hati za utambulisho mabalozi wa nchi mbali mbali

Rais Samia akutana na  Mabolozi wateule wa nchi mbalimbali Rais Samia akutana na Mabolozi wateule wa nchi mbalimbali

Rais Samia leo amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wateule wa nchi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini katika haflailiyofanyika Ikulu ya Jijini Dar es Salaam.

Hati hizo za utambulisho ni kutoka kwa Balozi Mteule wa Nigeria hapa nchini, Hamisu Umar Takalmawa, Balozi Mteule wa India nchini Biyana Srikanta Pradhan na Weibe Jakob De Boer ambaye ni Balozi Mteule wa Uholanzi hapa nchini.

Wengine ni Madina Diaby Kassamba Ganou ambaye ni Balozi Mteule wa Burkina Faso hapa nchini mwenye Makazi yake Nairobi, Kenya na Gaussou Touré, Balozi Mteule wa Guinea nchini mwenye Makazi Addis Ababa, Ethiopia.