Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 14Article 557431

Habari Kuu of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Rais Samia asisitiza umuhimu wa takwimu katika kutoa huduma

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema bila kuwa na hesabu au takwimu sahihi, haiwezekani kugawa rasilimali na kutoa huduma kwa Haki na uwiano

Amesema hayo leo Jijini Dodoma katika uzinduzi wa Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022.

Ameongeza kusema kwamba, ni ngumu kusghulikia masuala kama ya ajira, pasipo kuwa na idadi kamili ya wahitaji wa jambo husika.

"Huwezi kushughulikia changamoto ya Ajira endapo hujui watu wasio na Ajira. Huwezi kupeleka huduma na kushughulikia matatizo ya watu wenye mahitaji maalum kama Wazee na wenye Ulemavu"- Rais Samia