Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 20Article 572929

Siasa of Saturday, 20 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rais Samia atoa maagizo CCM

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wenyeviti wa mashina wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhimiza maendeleo kwa wananchi katika maeneo yao.

Ametoa wito huo jana wakati akizungumza kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa Shina Namba Moja Kata ya Kamunyika, wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, Juma Ahmed Rugina.

Rais Samia amezingumza na Rugina kwa simu ya mkononi ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ambaye alitembelea shina hilo kukagua uhai wa chama hicho.

Amepongeza balozi huyo kwa kuhudumu nafasi ya uenyekiti kwa miaka 20 mpaka sasa na kumuomba aendelee kuwafundisha wenyeviti wa mashina mengine kuhimiza uhai wa chama na maendeleo ya wananchi katika maeneo yao.

Pamoja na mambo mengine, Rais Samia amemuuliza Rugina endapo yeye pamoja na wananchi wa shina hilo wamechanja chanjo ya Covid-19 ili kujilinda na ugonjwa wa Covid-19.

Rugina amemueleza Rais kuwa wananchi wengi wamepata chanjo na kwamba wengine wanaendelea kuchanjwa.

“Huku chanjo zinaendela na vilevile tunaendelea kutumia vitakasa mikono,” Rugina alimjibu Rais huku akimshukuru kwa serikali yake kuendelea kuboreshea miundombinu ya barabara ikiwamo ujenzi wa barabara ambayo inaunganisha mkoa wa Kigoma na nchi jirani ya Burundi" amessema Rugani.

Rugina amemuomba Rais Samia kuwawekea makaravati na mifereji kwenye Barabara ya Kasulu Mjini ili kuzuia mmomonyoko wa udongo na kusababisha kuharibika wakati wa mvua.

Akijibu maombi hayo, Rais Samia amemwambia Rugina kuwa atamuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kasulu kuhakikisha makaravati hayo yanawekwa.