Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 23Article 573694

Habari Kuu of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rais Samia awashushia rungu zito askari barabarani

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia amewata askari wa barabarani kuzingatia misingi ya kazi zao ili kupunguza ajali za barabarani kwa kujenga urafiki na kuvaa hali ya usalama ili kuweza kutoa elimu ya usalama barabarani tofauti na kujenga uhasama baina yao na watumiaji wa barabara.

Ametoa kauli hiyo wakati akihutubia katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama leo Novemba 23, 2021 inayofanyika kitaifa jijini Arusha, na kurejelea takwimu zilizowakilishwa na Jeshi hilo kuhusu ajali za barabarani sambamba na vifo vitokanavyo na ajali hizo.

Rais Samia amewataka askari wa barabarani kujitahidi kujenga mazingira rafiki ili madereva na watumiaji wengine wakimbilie kwao pindi wanapopata tatizo barabarani tofauti na hizi sasa ambapo madereva wengi hukimbia pasipo kutazama usalama hivyo kusababisha ajali.

Aidha ametaja baadhi ya kero ambazo askari hao huzitengeneza hivyo kuchochea wimbi la ajali nyingi za barabarani na kulipunguzia hadhi jeshi hilo.

"Tabia ya kushikiria leseni muda mrefu si nzuri, na hii ya kulazimisha dereva alipe faini hapo hapo wakati sheria inatamka vizuri kuhusu muda wa kulipa faini hiyo, nendeni mshughulikie hayo" Amesema Rais Samia.

Ameongeza kusema kuwa vitendo vya ukamataji wa vyombo vya moto kwa wingi pasipo kusikiliza kesi hizo kunarudisha nyuma utendaji kazi kwa jeshi hilo sambamba na kurudisha nyuma maendeleo binafsi ya wamiliki wa vyombo hivyo.

"Vyombo vinakamatwa vingi vinaachwa hapo na vingine ukivitazama unaona vina miaka mingi, vinachakaa hapo, kama ushahidi upo kei isikilizwe naomba hili liangaliwe kwa undani" Rais Samia.