Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573445

Habari Kuu of Monday, 22 November 2021

Chanzo: mwananchidigital

Rais Samia awatunuku kamisheni maofisa 118 wa JWTZ

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan amewatunuku vyeo vya luteni usu maofisa 118 wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli mkoani Arusha.

Rais Samia leo ni mara yake ya kwanza kutunuku kamisheni katika chuo hicho Monduli tangu kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania.

Katika wahitimu hao, 99 ni wanaume na 19 ni wanawake ambapo kabla ya kutunukiwa kamisheni walishiriki katika gwaride na kula kiapo.

Awali Mkuu wa Chuo hicho, Brigedia Jenerali Jackson Mwaseba amesema wahitimu hao walikuwa katika makundi mawili ambapo walianza mafunzo mwaka 2018 baadhi ya ndani na nje ya nchi katika sayansi ya kijeshi ikiwepo wanajeshi wa anga.

"Katika kundi hili kuna marubani 56 na ufundi wa ndege ambao wamepata mafunzo ndani na nje ya nchi" amesema.

Viongozi mbalimbali wa Serikali na JWTZ wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo wameshiriki.