Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 28Article 560215

Habari Kuu of Tuesday, 28 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Rais Samia kuondoa ushuru taasisi za dini

Rais Samia kuondoa ushuru taasisi za dini Rais Samia kuondoa ushuru taasisi za dini

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ameshatoa maagizo kufanyika tathmini upya kwa taasisi za kidini nchini kubaini zile zinazofanya biashara na ambazo zinatoa huduma ili kuziondolea ushuru.

Rais Samia amesema hayo wakati wa sherehe ya miaka 50 ya Kanisa la Anglikana iliyofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John mjini Dodoma.

Akizungumzia maswala ya ushuru Rais Samia amesema Serikali itakuwa tayari kuondoa ushuru kwa taasisi za kidini ambazo hazifanyi shughuli zao kwa faida.

“Taasisi za kidini ambazo hutoa elimu na huduma za afya zinapaswa kuzingatiwa. Tuliangalia suala hili na kugundua kuwa viwango vinavyotozwa na taasisi za kidini katika afya na elimu sio tofauti sana na zile zinazotozwa na sekta binafsi, kwa hivyo dhahiri, pia zina faida,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais amesema kuwa kwa taasisi hizo za kidini ambazo zinapata faida kutokana na huduma zao kwa jamii zitaendelea kulipa ushuru na kuchangia Serikali.