Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573322

Habari Kuu of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rais Samia kutunuku kamisheni za kijeshi leo

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

RAIS Samia Suluhu Hassan leo Novemba 22, 2021 anatarajia kutunuku kamisheni katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Rais Samia angewasili jijini humo jana mchana akitoka Zanzibar.

Aidha leo jioni Rais Samia anatarajiwa kuzindua hoteli ya Gran Melia jijini humo.

Na hapo kesho Novemba 23, 2021 asubuhi Rais Samia atatarajiwa kufungua maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani katika uwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Baada ya ufunguzi huo Rais Samia anatarajiwa kuondoka mkoani humo.