Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 15Article 557617

Habari Kuu of Wednesday, 15 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Rais mwanamke tutamuweka 2025" - Rais Samia

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, watamuweka Rais Mwanamke ili kuondoa dhana iliyojengeka kwa miaka mingi kuwa wanawake hawawezi.

Ameyasema haya katika Maadhimisho ya siku ya Demokrasia nchini yanayifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Septemba 15 mwaka 2021, amesisitiza jambo hili kwa kusemakuwa ni kwa nguvu za Mungu jambo hilo litafanikiwa.

"Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana tukimuweka rais wetu tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana, wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti Samia hatasimama nani kawaambia"

"Kufika hapa bila kudra za Mwenyezi Mungu ni ngumu sasa, tungefikia hapo tunaenda tunarudi ni hapo hapo, sasa ndugu zangu niwaambie, Rais mwanamke tutamuweka 2025"- Rais Samia.

Katika uongozi wa Rais samia, kumeshuhudiwa mgawanyo wa madaraka kwa kufuata usawa wa kijinsia, hasa katika teuzi za viongozi wa juu ambazo amefanya hivi karibuni, kwa kuwateua wanawake kushika nafasi za juu katika kuongoza taifa hili.

“Fadhila za Mungu zikija mikononi mwako usiziachie, hizi ni fadhila za Mungu, wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii katika kujenga siasa, tumebeba wanaume katika siasa za nchi, leo Mungu ametupatia baraka, tukiiachia Mungu atatulaani,” Rais Samia Suluhu Hassan