Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 12Article 585229

Habari Kuu of Wednesday, 12 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Ratiba ya Mazishi Wanahabari Waliofariki kwa Ajali

Ratiba ya Mazishi Wanahabari Waliofariki kwa Ajali Ratiba ya Mazishi Wanahabari Waliofariki kwa Ajali

Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel inasema kuwa baada ya Ibada Maalumu ya kuwaaga Marehemu wa ajali ya Maafisa Habari na Waandishi waliofariki Jumanne kukamilika katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. Taratibu zitakazofuata zitakuwa kama ifuatavyo; 1. Mazishi ya Mwili wa Husna Mlanzi yatafanyika leo saa 10 jioni jijini Mwanza. 2. Mwili wa Antony Chuwa utasafirishwa kwa gari kwenda Moshi. 3. Mwili wa Johari utasafirishwa kwa gari kwenda Arusha. 4. Mwili wa Abel Ngapemba utasafirishwa kwa ndege kwenda Dar es Salaam; na 5. Mwili wa Steven Msengi utasafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa gari.