Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 16Article 557980

Habari Kuu of Thursday, 16 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Rugemalira Afika Kanisani Kumshuku Mungu

Rugemalira Afika Kanisani Kumshuku Mungu Rugemalira Afika Kanisani Kumshuku Mungu

MFANYABIASHARA maarufu nchini ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP na aliyekuwa mmiliki mwenza wa IPTL, James Rugemalira na familia yake wamefanya ibada ya shukrani katika Kanisa Katoliki Parokia ya Makongo Juu jijini Dar es salaam baada ya mahakama kumuachiwa huru.

Hii ni muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumuachia huru Rugemalira ikieleza kuwa mkurugenzi wa mashtaka nchini Tanzania (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi hiyo ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ulioisababishia hasara Serikali ya Tsh bilioni 358 iliyoanza kusikilizwa mahakamani hapo tangu Juni, 2017.