Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 07Article 583984

Habari Kuu of Friday, 7 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Rushwa, Fitina, Kunyanyasa Dada Zenu Marufuku

Rais Samia Rais Samia

RAIS Samia Suluhu, amepiga marufuku rushwa na udhalilishaji wa wagombea wanawake katika chaguzi za vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza katika kilele cha matembezi ya miaka 58 ya Mapinduzi, yaliyofanyika visiwani Pemba, Rais Samia amesema katika chaguzi vijana wa kike ndio wamekuwa wahanga wakubwa na kupiga marufuku unyanyasaji, rushwa na fitna.

“Vijana katika chaguzi zenu kunatawala fitina na rushwa, ikifika chaguzi za vijana sisi wenye watoto wa kike viroho juu, acheni kunyanyasa dada zenu, anayesimama anasifa apewe nafasi, yale mliyoyazoea acheni, simu siku moja unapokea 100,” amesema na kuongeza.

“Niwaombe vijana chaguzi zetu za jumuia, zinasimamiwa na kanuni na miongozo, vijana mna haki zote za kuchagua na kuchaguliwa, nendeni kagombeeni na mimi nawahakikishia, zitakapokuja juu tutatizama uwezo, weledi na si sura.