Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 30Article 540604

Habari Kuu of Sunday, 30 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

SIMBACHAWENE ASEMA WAHALIFU HAWATASHINDA

SIMBACHAWENE ASEMA WAHALIFU HAWATASHINDA SIMBACHAWENE ASEMA WAHALIFU HAWATASHINDA

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa corona ambayo inatarajiwa kutolewa nchini ni hiari na hakuna mtu atakayelazimishwa kufanya hivyo.

Dk Mwinyi alisema hayo akiwa Mahonda, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ziara ya kuwashukuru wananchi wa mkoa huo baada ya kukichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushika hatamu ya kuongoza dola katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Alisema serikali italeta chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 lakini itakuwa hiari kwa mtu anayehitaji na si lazima kama baadhi ya wananchi wanavyodai kiasi cha kuzusha taharuki.

Alitoa mfano kwamba, chanjo itatolewa kwa mahujaji wanaotarajiwa kufanya ibada ya hijja Makka, Saudi Arabia ambayo ni sehemu ya masharti ya serikali hiyo kwa mahujaji watakaotekeleza ibada ya hijja ili kupunguza uwezekano wa kuibuka kwa mripuko wa maradhi hayo.

“Ndugu wananchi napenda kuweka wazi na bayana suala hili...chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa corona ni hiari na hakuna atakayelazimishwa ingawa kwa upande wa mahujaji serikali ya Saudi Arabia wametutaka mahujaji watakaofanya ibada hiyo lazima wapewe chanjo,’’ alisema.

Awali, Dk Mwinyi alisema katika kipindi cha miezi sita aliyepo madarakani amefanikiwa kujenga nidhamu na uwajibikaji na kuweka vizuri misingi ya matumizi ya fedha za umma.

Alisema katika kipindi cha miezi sita amefanya mambo makubwa matatu ikiwamo kujenga mshikamano wa wananchi wa Zanzibar kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa yenye lengo la kuleta maridhiano ya kisiasa.

Mwinyi alisema maridhiano hayo yamefungua milango ya wananchi kuelewana na kuondosha siasa za chuki na uhasama zilizokuwepo ambazo kwa kiasi kikubwa zilirudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

“Huwezi kupata maendeleo kama wananchi wako hawana amani...wanagombana na kujenga chuki na uhasama katika kipindi cha miezi sita tumefanikiwa kuwaunganisha wananchi wote na sasa wanafanya kazi pamoja na kuweka pembeni tofauti zao”alisema.

Aidha alisema katika miezi sita amekuwa akifanya kazi kuweka vizuri mifuko ya ukusanyaji wa kodi ambayo haikuwa vizuri na chanzo kikuu kikiwa upotevu wa mapato.

Alitoa mfano wa mapato yanayovuja katika taasisi akisema Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO) halifanyi vizuri katika makusanyo kwa sababu hakuna mifumo mizuri.

Alisema malengo yaliyowekwa ambayo yamo katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ikiwemo ujenzi wa bandari na miundo mbinu yake , tayari wawekezaji wapo wanasubiri.

Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Iddi Ame Haji alimpongeza Rais Mwinyi kwa kuanza vizuri katika uongozi wake wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) awamu ya nane.

Join our Newsletter