Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 06Article 541258

xxxxxxxxxxx ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

SMZ YATENGA BIL 7/- KUSAIDIA MABARAZA YA VIJANA

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetenga Sh bilioni saba kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya mabaraza ya vijana kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi na kujiajiri.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Tabia Mwita Maulidi wakati akijibu hoja mbali mbali za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochangia bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2021-2022.

Alisema mabaraza ya vijana, yalianzishwa zaidi ya miaka mitatu sasa, lakini bado vijana wengi hawana mwamko wa kujiunga na kufanya kazi za ubunifu .

Jumla ya vijana 18,364 wamejiunga na mabaraza ya vijana Zanzibar ambayo yameundwa kwa ajili ya kuwaunganisha vijana kufanya kazi za ujasiriamali.

Akifafanua zaidi alisema maeneo mbalimbali yametengwa kwa ajili ya shughuli za kazi za ujasiriamali kwa vijana waliojiunga na mabaraza ya vijana ikiwemo Bumbwini, Panga tupu pamoja na Bambi kwa upande wa Unguja.

Mwita alisema lengo la serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ya awamu ya nane ni kuwataka vijana kujitegemea na kuwa wajasiriamali kwa ajili ya kujiajiri.

Join our Newsletter