Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 19Article 558280

Diasporian News of Sunday, 19 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

SMZ kuunda mamlaka madhubuti kukabili dawa za kulevya

SMZ kuunda mamlaka madhubuti kukabili dawa za kulevya SMZ kuunda mamlaka madhubuti kukabili dawa za kulevya

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaunda mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya yenye uwezo wa kukamata watuhumiwa kufanya upelelezi pamoja na kuwafi kisha mahakamani.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais, Hemed Suleiman Abdalla, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu nia ya serikali kuwasilisha muswada wa marekebisho ya sheria ya dawa ya kulevya.

Alisema Sheria ya Tume ya Kuratibu na Kupambana na dawa za kulevya iliyopo sasa haina meno ya kuweza kufanya kazi za upelelezi wa masuala ya dawa za kulevya ikiwemo kukamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani.

Aliongeza kuwa hivi sasa kazi zote hizo zinafanywa na Jeshi la Polisi ambalo limeibua malalamiko mengi kwa wananchi katika kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na uaminifu wa hali ya juu.

Alisema utafiti uliofanywa unaonesha kwamba kesi nyingi zinazofikishwa polisi hulazimika kufutwa kwa kukosa ushahidi pamoja na zile zinazokwenda mahakamani kukosa uthibitisho kwa watuhumiwa.

Aliwataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kujipanga kupokea muswada wa marekebisho ya sheria ya dawa za kulevya na kuuchangia kwa ajili ya kuupa uwezo zaidi katika mapambano hayo.

Abdalla ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Kupambana na Dawa za kulevya Zanzibar, alisema wamejipanga kuhakikisha doria zinafanyika mara kwa mara katika maeneo ya ukanda wa bahari ya visiwa vya Unguja na Pemba.

Alisema utafiti uliofanywa umebaini kwamba wahalifu wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia bandari bubu kuziingiza pamoja na kusafirisha bidhaa mbalimbali.

Alitoa mfano kwamba, zipo zaidi ya bandari bubu 271 Unguja na Pemba ambazo hutumika kusafirisha na kuingiza bidhaa mbalimbali kinyume na sheria bila ya ukaguzi.

“Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi tunategemea kuwasilisha sheria ya mabadiliko ya tume ya dawa za kulevya ambayo hiyo itaunda mamlaka ya kudhibiti yenye uwezo kamili, ...tunawaomba tukileta sheria hiyo muwe tayari kuichangia,” alisema