Uko hapa: NyumbaniInfos2020 09 25Article 510391

Crime & Punishment of Friday, 25 September 2020

Chanzo: HabariLeo

Saba mbaroni kwa madai ya kutorosha bilioni 7.2 nje ya nchi

Saba mbaroni kwa madai ya kutorosha bilioni 7.2 nje ya nchi

Taasisi ya Kupamba na Kuzuia Rushwa Nchini (TAKUKURU) imewatia mbaroni wafanyabiashara maarufu saba wa madini ya Tanzanite mkoani Arusha kwa tuhuma ya kumiliki mali na fedha taslimu zaidi ya Sh bilioni 7.2 bila ya kuwa na maelezo ya kutosha ya upatikanaji wa utajiri huo na pia wamekuwa wakitorosha madini nje bila kufuata taratibu za kiserikali.

Akizungumza jijini Arusha leo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia John Mbungo aliwataja wafanyabishara hao ni pamoja na Joel Mollel maarufu kwa jina la ''Saitoti'' ambaye ni meneja wa kampuni maarufu ya Gem and Rock Venture ya Jijini Arusha.

Pia inamshikilia mke wa meneja huyp. Caren Mollel wote wanadaiwa kumiliki Sh bilioni 5.5 kinyume na utaratibu.

Wengine waliotajwa ni Mtanzania Rakesh Kumar Gokhroo anayemiliki kampuni ya Colour Clarity ya Jijini Arusha.

Pia wanamshikilia Daud Lairumbe ambaye ni wakili wa kampuni ya Gem and Rock Venture kutoka kampuni ya uwakili ya Northen Law Chambers Advocates & Legal Cunsultants ya Jijini Arusha sambamba na George Kivuyo ambaye ni mshirika wa kampuni hiyo.

TAARIFA ZAIDI FUATILIA GAZETI LA HABARILEO KESHO

Join our Newsletter