Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 20Article 572965

Habari Kuu of Saturday, 20 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Sababu za Kamala Harris kuwa Rais kamili kwa dakika 85

Sababu za Kamala Harris kuwa Rais kamili kwa dakika 85 Sababu za Kamala Harris kuwa Rais kamili kwa dakika 85

Jana November 19, 2021, Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris alikua Rais kamili wa nchi hiyo wa muda dakika 85 (saa 1:25).

Sababu za kutokea jambo hilo ni kutokana na Rais Joe Biden kwenda kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo. Rais Biden alikabidhi mamlaka ya Urais kwa Kamala kwa muda wa dakika 85 ambazo alizitumia kufanya uchunguzi wa kiafya.Uchunguzi huo umekuja siku chache baada ya Joe kuonekana akipata shida ya kukohoa wakati akiongea. Na hivi karibuni baadhi ya wananchi walionesha wasiwasi juu ya Afya ya Rais hiyo kupelekea kufanyiwa uchunguzi ambao ripoti yake imewekwa hadharani na Daktari wa Ikulu ya Marekani.

Afya ya Biden kwa mujibu wa Daktari iko salama na anaweza kuendelea na majukumu yake kama Mtendaji Mkuu, Rais wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu.