Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 13Article 557182

Habari Kuu of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Sababu za Rais Samia kutenganisha Wizara ya Habari

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan ametaja sababu ya kuihamishia idara ya Habari katika Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuwa ni kwa ajili ya kuitimiza wizara hiyo

Amefafanua kuwa amefikia maamuzi hayo mara baada ya wadau wa Habari kupeleka maoni mengi kuomba Wizara hiyo ya mawasiliano na teknolojia kuwa na habari ndani yake.

"Nimechukua habari nimeipeleka ilipokuwa mawasiliano na teknolojia, ili kuitimiza, yale maneno 'habari habari' kuwa sehemu moja, na nina imani kuwa hivyo itawasaidia kufanya kazi vizuri" Rais Samia

Awali Sekta ya Habari ili kuwa chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Saana na Michezo kabla ya kuhamishiwa kwenye Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia.

Aidha mabadiliko haya katika Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia yameambatana uteuzi mpya wa Waziri kutoka kwa Dk.Faustine Ndugulile kwenda kwa Dk.Ashatu Kijaji.