Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 10Article 584740

Muziki of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Sababu za mafanikio ya Shatta Wale ni hizi.....

Sababu za mafanikio ya Shatta Wale ni hizi..... Sababu za mafanikio ya Shatta Wale ni hizi.....

Mwanamuziki wa dancehall kutoka nchini Ghana Shatta Wale amefunguka kuhusu undani wa chanzo cha mafanikio yake na kinachomfanya kuwavutia mashabiki wengi wa muziki wake nchini humo.

Mara kadhaa mashabiki zake wamekuwa wakifurika katika kila sehemu anayokuwapo ili kumshuhudia msanii huyo.

“Ni Mungu tu, kwa sababu sauti ya watu ni sauti ya Mungu. Watu wanasema mambo mengi sana kuhusu mimi lakini unavyonifikiria, wengine hawaoni hivyo kuna mtu fulani anataka kumuunga mkono Shatta Wale bila kujali, hivyo nikienda mahali, hizo roho zinaungana.” alisema.

Shatta Wale anabainisha kuwa anaamini sana mapenzi anayopata kutoka kwa mashabiki wake, kiasi cha kuamua kuwarushia Pesa mitaani kwa madai ya kurejesha kwa jamii.

Jambo hilo lilipingwa vikali na baadhi ya wadau nchini humo kwa madai ya kuwa hapaswi kurusha pesa badala yake alitakiwa kuwagawia kwa utaratibu mzuri kama itolewavyo zaka au sadaka.

“Nimejiambia kuwa siku yoyote ile zaka nitakayoipeleka kanisani ni bora niinyunyize mitaani,” alisema akijibu tuhuma za waliokosoa vikali.