Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 15Article 551623

Uhalifu & Adhabu of Sunday, 15 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Sabaya kuendelea kujitetea Jumatatu

Sabaya kuendelea  kujitetea Jumatatu Sabaya kuendelea kujitetea Jumatatu

MSHITAKIWA wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha, Lengai Ole Sabaya (34) ataendelea kujitetea kesho (Jumatatu) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha.

Katika kesi hiyo, Sabaya na wenzake wawili, Silvester Nyengu (26) na Daniel Mbura (38) wanadaiwa kutumia silaha na kupora mali na Sh 3, 159,000 katika duka la Shahiid Store kwenye mtaa wa Bondeni, jijini Arusha.

Washitakiwa hao walidaiwa kufanya hivyo Februari 9, mwaka huu saa 11 jioni wakati Sabaya akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.

Ilidaiwa mahakamani kuwa, kabla ya kupora, washitakiwa hao waliwashambulia watu kadhaa kwa ngumi, mateke, makofi na kichwa.

Sabaya kesho (Jumatu Agosti 16,2021) atatoa ushahidi akiongozwa na mawakili wake, Dancan Oolla na Mosses Mahuna.