Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 12Article 551128

Uhalifu & Adhabu of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: Tanzaniaweb

Sabaya na wenzake wakutwa na kesi ya kujibu

Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai na Wenzake Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai na Wenzake

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imethibitisha kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, Sylvester Nyegu pamoja na Daniel Mbura, wana kesi ya kujibu katika kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, amesema baada ya kusikiliza ushahidi wote uliotolewa na upande wa mashtaka, mahakama imebainika kuwa washtakiwa wote kwa pamoja wana kesi ya kujibu.

Hakimu Amworo anayesikiliza kesi hiyo amewaambia washtakiwa kwamba wanaruhusiwa kujitete mahakamani hapo kwa njia ya kiapo au bila kiapo,

Aidha mahakama imewataka washtakiwa kutaja idadi ya mashahidi na vielelezo watakavyo kuwa navyo, na kwamba utetezi wao utaanza kusikilizwa hapo kesho.

Watuhumiwa hao wanashitakiwa kwa makosa matatu, ikiwemo unyang'anyi wa kutumia silaha na wizi wa kutumia silaha, ambapo kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo July 16 na kuanza kusikilizwa July 19 mwaka huu.