Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573532

Habari Kuu of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Sakata la Mgao wa Maji, Aweso Atua Site

Sakata la Mgao wa Maji, Aweso Atua Site Sakata la Mgao wa Maji, Aweso Atua Site

Serikali imedhamiria kutumia zaidi ya Bilioni 390 kujenga Bwawa la kuhifadhia maji katika kijiji cha Kidunda wilayani Morogoro Vijijini, kama akiba ya Mto Ruvu ambao ndio chanzo kikubwa cha huduma ya Maji kwa Mikoa ya Pwani na Dar es salaam.

Bwawa hilo linategemea kuwa na urefu wa mita 860 na kimo cha mita 21 na uwezo wa kuhifadhi maji Lita Billioni 190.

Maji haya kwa sehemu kubwa husababisha mafuriko wakati wa mvua za masika na hivyo yakihifadhiwa kwenye Bwawa la kidunda itasaidia tatizo la upatikanaji wa maji wakati wa kiangazi.

Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso ambaye ametembelea kuona na kujiridhisha eneo la utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati, amesema kuwa Serikali imeshalipa fidia ya Billioni 12 kwa wananchi wa eneo la Kidunda waliopisha ujenzi wa Bwawa hilo na tayari wananchi wameshaondoka eneo la mradi ili kupisha ujenzi wa Bwawa.