Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 16Article 542965

Habari Kuu of Wednesday, 16 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Sakata maduka kubadili fedha laibuka bungeni

Sakata maduka kubadili fedha laibuka bungeni Sakata maduka kubadili fedha laibuka bungeni

Amesema jimboni kwake wafanyabiashara hao sasa wanateseka na kuhoji kama kuna watu serikalini wanataka kuifanya biashara hiyo.

Akichangia juzi bungeni jijini Dodoma mapendekezo ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22, mbunge huyo alisema kuwa jijini Arusha wamepata shida na kuteseka kutokana na vikosi ambavyo kila siku vimekuwa vikishindana kwenda huko.

“Vikosi hivi baadaye vikaja na mambo haya ya maduka makubwa ya kubadilishia fedha na watu wa maduka haya kuna mchezo wanaucheza ambao sijui watu wa serikali kuna ambao wanataka wafanye hii biashara, maana ukiangalia Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2015 mtaji wa mtu wa maduka haya ulikuwa Sh. milioni 40,  wakaja mwaka 2017 wakaongeza Sh. milioni 100.

“Mwezi Mei mwaka 2018, wakaongeza hadi Sh. milioni 300, baadaye wakaona kila wakiongeza wale wanafanya biashara, baadaye wakaamua kuvamia na kwenda kuwapora.

"Wakapora fedha zao, wakapora magari yao, wakapora hati zao za nyumba, wakapora viwanja, wamebaki hoi, hili tatizo ni kubwa," alilalamika.

Februari 2018, Meneja wa Kitengo Kinachosimamia Fedha za Kigeni katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Eliyamringi Mandari, alisema BoT imeyafungia baadhi ya maduka.

Alibainisha kuwa Desemba maduka 63 yaliomba kusajiliwa upya ambayo leseni zao zilifutiwa na yaliyobaki kati ya 297, maombi yao yaliendelea na wengi waliyapeleka karibia mwishoni na walitoa mwezi mmoja kuyapitia na kutaka kama kuna nyongeza wazipeleke kabla ya Januari 31.

Alisema ilipofika mwezi huo mchakato huo ulifungwa lakini yapo maduka 65 maombi yao yalikuwa yanafanyiwa kazi.

“Hadi kufika mwisho wa tarehe hiyo  maduka takribani 71 yalipewa leseni yakiwa na nyongeza ya matawi 40, hivyo jumla yakawa 111,” alisema.

Aliongeza kuwa mpaka wakati huo wakizungumza, maduka 86 yalifutiwa leseni zao kwa kutotimiza masharti ikiwa ni pamoja na kutokuomba.

“Maduka 34 yaliomba kujitoa kwa sababu zao za kutotimiza hayo masharti, na kati ya maduka 86 mengi hayakuleta maombi na yaliyoleta yakashindwa kutimiza masharti, sharti kubwa ni namna ya kujieleza na kutoa viambatanisho sahihi vya fedha wanazotaka kuwekeza kwenye biashara hii zimepatikana kwenye vyanzo vipi,” alisema.