Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573526

Habari za Mikoani of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Same yapokea Sh2.6 bilioni za miradi ya maendeleo

Same yapokea Sh2.6 bilioni za miradi ya maendeleo Same yapokea Sh2.6 bilioni za miradi ya maendeleo

Halmashauri ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro imepokea Sh 2.6 bilioni kutoka Serikali Kuu kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa 56 katika shule za sekondari ndani ya Wilaya hiyo.

Fedha hizo ambazo zimekuja nje ya bajeti ya Halmashauri hiyo ni pamoja na za Covid-19 amazo ni Sh1.1 bilioni ambazo zimeelekezwa kwenye ujenzi wa madarasa 56 katika shule za sekondari.

Akizungumza leo Jumatatu Novemba 22, 2021 katika kikao cha baraza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Annastazia Tutuba amesema fedha hizo zimekuja wakati muafaka kwani zitasadia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

Tutuba amesema changamoto ya madara kwenye Wilaya hiyo kwa kiasi kikubwa imepatiwa utatuzi baada ya kupokea fedha hizo ambazo zimesukuma gurudumu la maendeleo ya elimu kwa jamii.

"Tumepokea pesa hizi toka Serikali Kuu kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mwaka huu na pesa hizi zimekuja nje ya bajeti ya Halmashauri yetu na tunaipongeza Serikali kwakutupatia fedha hizi ambazo sasa zinaenda kupunguza mzigo wa miradi ya maendeleo kwa wananchi" amesema Tutuba

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Yusto Mapende amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kushirikiana na watendaji wa vijiji na kata katika kusimamia ipasavyo fedha hizo ili miradi ya maendeleo itekelezwe kwa wakati na kwaufanisi.

Mapande amesema changamoto iliyopo ni baadhi ya watendaji wa Serikali wasio waadilifu katika utendaji wao wa kazi hivyo kutoa rai kwa Madiwani kuhakikisha wanasimamia vyema pesa hizo.

"Tumepokea pesa hizi toka Serikali hii ni kuonyesha namna inavyowajali wananchi wake jambo la msingi hapa ni kuhakikisha kila kiongozi anasimama vyema kwenye nafasi yake" amesema Mapande

Fedha hizo zinatarajiwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa pamoja na vituo viwili vya Afya sambamba na kuikarabati miundombinu ya madarasa pamoja na Zahanati.