Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585475

Habari Kuu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Samia Ampa Kazi Hii Lukuvi

Samia Ampa Kazi Hii Lukuvi Samia Ampa Kazi Hii Lukuvi

RAIS Samia Suluhu Hassan, amempa jukumu aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe William Lukuvi la kuunganisha Wizara zote na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta ufanisi zaidi.

Samia ameyasema hayo leo Januari 12, 2022 kwenye Mkutano wake Maalum na Mawaziri na Manaibu Waziri uliofanyika katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma na kuongeza kwamba, amesema Lukuvi atamsaidia Waziri Mkuu kushughulikia wizara zote.

"Mara kadhaa tulikuwa tunazungumzia masuala ya kufanya kazi kila Mtu na lake hakuna uratibu, hakuna coordination ndani ya Sekta zenyewe na hata baina ya Sekta na Sekta, kila Mtu anafanya lake mwisho wa siku unakuja kutafuta outcome ya suala lililofanywa kula mtu anakupa kipandekipande na huoni uzito wake.

Nadhani upande wa Waziri Mkuu ambao Mh. Lukuvi atakuja kutusaidia kwenye hilo, uratibu wa Sekta Wizara mbalimbali na Taasisi za Serikali.

"Katika kufanya kazi zetu kuna kiungo cha katikati mbali na Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu lakini pia kuna Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi na yenyewe kuna aina ya kutuunganisha na ana majukumu makubwa ya kuangalia hasa katika level ya utendaji, tutakuwa tunaratibiwa chini ya Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi," amesema Rais Samia.