Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 26Article 544429

Habari Kuu of Saturday, 26 June 2021

Chanzo: ippmedia.com

Samia:Tumeanza mazungumzo mradi Bandari ya Bagamoyo

Samia:Tumeanza mazungumzo mradi Bandari ya Bagamoyo Samia:Tumeanza mazungumzo mradi Bandari ya Bagamoyo

Rais Samia ameyasema hayo leo wakati wa Mkutano wa Baraza la Taifa la biashara uliofanyika ikulu Jijini Dar es Salaam huku akidokeza kufufuliwa kwa miradi mingine ya mchuchuma na liganga.

“Naomba niwape taarifa njema kwamba tumeanza mazungumzo upya ya kufufua mradi wa bagamoyo ,pamoja na mchuchuma na liganga nilishatoa maelekezo nadhani sekta husika zinaendelea” amesema Rais Samia.

“Na mazungumzo na wawekezaji wa mchuchuma na liganga kuona tatizo ni nini hasa, Serikali inaweza kujitoa mpaka wapi na muwekezaji anaweza kujitoa mpaka wapi na taarifa zilizopo duniani ni kwamba chuma imepanda bei” aliongeza

Mradi huo umeukuwa ukiibua hoja kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo wabunge wengine wakiukubali huku wengine wakiupinga kwa madai kuwa unaweza kuwa na faida zaidi kwa muwekezaji kuliko wananchi.