Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585436

Habari Kuu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Samia aonya ajira za kindugu, "Mtaua Taasisi!"

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Samia, amewaonya viongozi wenye tabia ya kuajiri ndugu, rafiki, jamaa kinyume na taratibu za Utumishi wa Umma kwa madai ya kufahamiana kwani vitendo hivyo vinashusha utendaji kazi na kurudisha nyuma maendeleo ya taifa.

Ametoa onyo hilo mapema hii leo Januari 13, 2022 wakati akizungumza katika kikao chake cha Mawaziri pamoja na Manaibu Waziri kilichofanyika Jijini Dodoma.

Samia amekemea tabia hiyo hasa kwa wale wenye michezo ya kuwapachika ndugu ambao hawana vigezo, sifa wala weledi wa kazi husika kwa kisingizio cha kujuana, kukua, kusoma eneo moja.

"Kuna hizi ajira za kindugu, kirafiki hizi zinaharibu utendaji wa kazi, natambua kuwa kuna baadhi ya marafiki wanakuwa na uwezo wa kazi hizo na unajua kabisa ukiwaweka basi watafanya makubwa hii ni sawa lakini sio mnavutana tu huko eti tumezaliwa sehemu moja, tumekua wote mara tunaishi eneo moja, jamni mtaua Taasisi! amesisitiza Rais Samia.

Aidha amewataka viongozi wote kusimamia maadili ya kazi ili kuweza kufikia malengo makuu ya Serikali yaliyowekwa kwa mutakabali wa taifa kwa ujumla.