Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 10Article 584623

Habari Kuu of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Samia asafisha hali ya hewa 'Lukuvi na Kabudi' kuachwa Baraza jipya

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Baada ya Rais Samia kufanya mabadiliko katika Braza la Mawaziri, yapo mengi yaliyoibuka juu ya wale waliotemwa katika uteuzi wa Mawaziri hasa aliyekua Waziri wa Ardhi, William Lukuvi na Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Kabudi kutolewa katika Baraza la Mawaziri jipya lilioundwa na Kiongozi huyo mkuu wa nchi.

Akizungumza wakati wa hafla ya uuapishwaji wa Mawaziri, Manaibu Waziri, Majaji na wenyeviti wa Tume mbalimbali, Rais Samia mapema leo Januari 10, 2022 amesema kua viongozi hao wawili hawapo kwenye Baraza la mawaziri kwakuwa wana kazi ya kufanya na yeye.

Samia amesema kuwa lengo kuu la kuwaondoa viongozi hao katika Baraza la mawaziri ni kwasababu anataka kufanya nao kazi kwa ukaribu ikiwa ni pamoja nakuwasimamia mawaziri wapya walioteuliwa ambao wengi wao bado ni vijana.

"Ukiwatizama hawa ni kaka zangu, kuwaacha kwenye list ni kuwavuta waje kwangu, na hawa walioteuliwa wote ni wadogo wadogo, hivyo nimewaacha wawasimamie" Rais Samia

Majukumu mapya ya Kabudi

Akizungumza kuhusu majukumu mapya aliyompangia Prof Kabudi, amesema kuwa kiongozi huyo amefanya kazi kubwa katika kusimamaia mikataba mingi ya kitaifa hivyo hivi sasa atahudumu katika kitengo cha katiba na makubaliano ambacho amekitaja kuwa sio rasmi kwa kutangazwa.

Kuhusu Lukuvi.

Rais Samia amesema kuwa kuna minongono mingi inayoendelea katika mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na jumbe za maandishi zilizotengenezwa kwa nia ya kumchafua kiongozi huyo ambaye amemtaja kama mchapakazi imara aliyefanya makubwa ndani ya Wizara ya Ardhi.

Amesema kuwa siku si nyingi atatangaza majukumu mapya ya kiongozi huyo huku akisawazisha hali ya hewa kwa kuwakata kilimi wale wote wanaoendelea uvumi kuwa Lukuvi amejipanga kuwania nafasi ya uspika kuwa jambo hilo halipona kuwa kiongozi huyo anayo kazi maalum.

"Kuna wale waliosema bora Lukuvi katoka, niwambie tu kuwa hajatoka, na ale wanaosema anagombania uspika niseme tu kuwa hata gombania uspika! huyu ana kazi na mimi na siku si yingi nitaitangaza"